Mbwana Samatta usiku wa August 23 2018 aliingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kufunga hat-trick yake ya kwanza akiwa Europe akiichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji, Samatta aliifunga hat-trick hiyo katika ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Brondby IF mchezo wa kuwania kucheza hatua ya Makundi UEFA Europa League.
Samatta baada ya hat-trick hiyo alifanya mahojiano maalum na Genk TV na ilikuwa hivi “Sijui ni jina gani jipya la utani naweza kujiita lakini siku zote nimekuwa nikipewa AKA na mashabiki na siwezi kukataa lakini nafikiri jina la Sama Goal linatosha”
“Ndio nilikuwa naamini nikianza kufunga nitakuwa na funga kwa sababu naamini ubora wangu na najituma sana nikiwa katika timu na ikitokea nikipata goli inakuwa kama ni bonus kwangu kwa sababu siku zote nimekuwa nikipenda kushinda na kusaidia timu yangu kupata matokeo”
“Hatukushangazwa na Brondby IF kipindi cha pili kubadilika kwa sababu ni wazuri lakini hatukuamini kama wangeweza kufunga magoli mawili ndani ya dakika tano, tulikuwa tunafikiri tunaweza kuanza tena na kuutawala mchezo lakini hatukuwa na nafasi kwa wakati huo, hongera kwa timu kwa ujumla tutaenda katika mchezo wa marudiano kama timu na ikitokea nikapata nafasi mguuni kwangu nafunga”
Samatta hataki utani safari ya Europa League, leo kapiga hat-trick