Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtuma Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumwakilisha katika sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Dambudzo Mnangagwa zitakazofanyika kesho Jumapili tarehe 26 Agosti, 2018 katika uwanja wa michezo wa Taifa Mjini Harare.
Rais Mstaafu Dkt. Kikwete atafuatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Philip Japhet Mangula na Mwenyekiti wa chama cha UDP John Momose Cheyo.
Rais Mnangagwa ataapishwa kesho kuongoza Zimbabwe baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 30 Julai, 2018 akiwa anapokea kijiti kutoka kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Gabriel Mugabe.