Club ya KRC Genk ya Ubelgiji usiku wa August 26 2018, iliingia katika uwanja wake wa nyumbani Luminus Arena kucheza game yake ya tano ya Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Waasland Beveren.
KRC Genk inachezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta, ambaye leo katika mchezo huo inaonekana kocha aliamuwa kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake kama Leandro Trossard na Mbwana Samatta kwa ajili ya game muhimu ya marudiano ya UEFA Europa League kuwania kuingia makundi itakayochezwa Alhamisi ya August 30.
Samatta alitokea benchi katika mchezo huo dakika ya 59 na kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Zinho Gano wakati ambao KRC Genk ilikuwa sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Beveren, dakika ya 66 Beveren wakapata goli la pili dhidi ya KRC Genk, hali ikawa ngumu zaidi kwa Genk kupambana kusawazisha.
KRC Genk waliongeza kasi zaidi na dakika ya 78 Mbwana Samatta akafunga goli la kichwa na kuisawazishia Genk kabla ya dakika moja kabla ya game kumalizika Leandro Trossard kufunga goli la ushindi kwa Genk na kuufanya mchezo kumalizika kwa Genk kupata ushindi wa magoli 3-2, goli la kwanza la Genk likifungwa na Edon Zhegrova dakika ya 20.
Magoli pekee ya Beveren yalifungwa na Nana Opoku Ampomah dakika ya 66 na 75, ushindi huo sasa unawafanya Genk kuongoza Ligi kwa kuwa na jumla ya point 13 wakifuatiwa na Club Brugge wenye point 13 pia ila wametofautiana goli moja na Genk ambao katika game zao tano za Ligi hawajapoteza mchezo wowote wakishinda game nne na sare game moja.
Kwa kasi anayoenda nayo Mbwana Samatta anatabiriwa kuwa atafanya vizuri sana na Genk msimu huu, hiyo ni baada ya kufanikiwa kupambana na jeraha lake la goti miezi kadhaa nyuma, Samatta kwa sasa ana jumla ya magoli matatu Ligi Kuu msimu huu akicheza game nne kati ya tano, akiwa nafasi ya tano kwa wanaongoza kwa ufungaji magoli Ubelgiji, tofauti ya magoli manne na Santini wa Anderltch anayeongoza ila Samatta amefunga jumla ya magoli nane katika game tano zilizopita za mashindano yote za Genk.
NI KISANGA: Kama kucheka ni afya basi pata hapa (Yusufuuuu au Skriipapapaa)