Usiku wa August 27 2018 club ya Man United ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilicheza game ya tatu ya Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 dhidi ya Tottenham Hotspurs katika dimba lake la nyumbani Old Trafford.
Man United walikuwa nyumbani lakini walijikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-0, magoli ya Spurs yakifungwa na Harry Kane dakika ya 50 na Lucas Moura aliyefunga magoli mawili dakika ya 54 na 84, hivyo game ikamalizika ubao wa matokeo ukisomeka 3-0.
Baada ya game kocha wa Man United Jose Mourinho kama ilivyo kawaida yake akaongea na waandishi wa habari na kujibu maswali mbalimbali, Mourinho katika mkutano na waandishi wa habari alionekana kukasirika kutokana na maswali yao.
Mourinho alikasirishwa na kuondoka kati kati ya interview huku akisema “Peke angu nimeshinda mataji matatu ya Ligi Kuu zaidi ya makocha wote 19 EPL, wao kwa pamoja ndio wameshinda mawili ila mimi matatu niheshimu” kauli ambayo inaashiria kuwa Mourinho kwa sasa ndio kocha mwenye mafanikio zaidi EPL kati ya wote 19 waliobaki kwani amechuku EPL mara tatu.
Kipigo cha Tottenham Hotspurs kwa Man United ya Jose Mourinho ni kipigo cha pili mfululizo baada ya kipigo cha August 19 2018 dhidi ya Brighton Hove Albion cha magoli 3-2, wakiwa wamecheza jumla ya game tatu za EPL msimu huu na kuruhusu kupoteza game mbili na ushindi game moja, Man United kwa sasa wapo nafasi ya 13 kwa kuwa na point tatu.
Unaweza bonyeza PLAY kutazama Interview yenyewe
Kitu Manara kaandika kuhusu ishu za kufukuzwa kocha