Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji(ICSID) imeikataa rufaa ya TANESCO kupinga hukumu ya kuilipa Benki ya Standard Chartered takribani Tsh. Bilioni 338.8 (USD 148.4 Million)
Kutokana na hukumu hiyo, TANESCO inatakiwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa katika hukumu ya mwaka 2016.
Fedha hizo ni madai ya malipo ya umeme baina ya TANESCO na Kampuni ya IPTL iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura kuanzia Mei 26, 1995 huku ikidaiwa na benki hiyo.
IPTL ilikuwa ikidaiwa na benki hiyo ya Hong Kong kutokana na mkopo iliyochukua kutekeleza mkataba kati yake na TANESCO.
Aidha, TANESCO imeagizwa kulipa gharama zote za uendeshaji wa shauri hilo ikiwamo ada ya kesi na malipo ya wajumbe wa kamati waliolisikiliza.