Leo August 28, 2018 Taarifa ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na Makamu wake, Jitu Soni wamejiuzulu nafasi hizo leo.
Ghasia ambaye ni Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) na Soni Mbunge wa Babati Vijijini wametangaza uamuzi huo mbele ya Wajumbe wa kamati hiyo.
Aidha, Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai amethibitisha habari hizo ingawa sababu za viongozi hao kujiuzulu hazijafahamika bado.
Afisa Mdai kodi harusini kaibukia kwenye mechi CCM Kirumba