Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea club ya Juventus ya Italia kwa sasa Cristiano Ronaldo, goli lake Jumanne ya August 28 2018 ndio lilitangazwa kuwa goli bora la UEFA msimu wa 2017/2018.
Ronaldo goli lake alilolifunga dhidi ya Juventus msimu uliopita akiichezea Real Madrid ndio goli bora la UEFA na baada ya kushinda tuzo hiyo Ronaldo aliizungumzia ishu ya kufunga goli hilo.
“Niliona mpira ukiwa juu na nikasema ngoja nijaribu labda inawezekana nitashindwa kuugusa lakini najaribu, nilifanikiwa kuugusa na namna nilivyougusa ulienda moja kwa moja kwa nguvu katika goli, nilivyoanguka chini naangalia mpira huko nyavuni”
“Nikasema waooh!! nimefanikisha nilishikwa na mshangao lakini wakati huo huo sikushangazwa sana kwa sababu kwa muda mrefu nimekuwa nikijaribu kufunga goli katika robo fainali lakini kufunga katika game za kufuzu ni fahari sana”
Cristiano Ronaldo akielezea namna alivyoshinda goli bora la UEFA 2017/18 akiwa na Real Madrid dhidi ya Juventus, hakutarajia kama alivyoruka angeweza kuupata mpira #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ktoVpx6LvJ
— millardayo (@millardayo_) August 28, 2018
Kitu Manara kaandika kuhusu ishu za kufukuzwa kocha
d