Leo August 30, 2019 Kiongozi wa chama cha ‘Economic Freedom Fighters (EFF) cha nchini Afrika Kusini Julius Malema ametaka bara la Afrika lianze kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha kuu katika mawasiliano.
Malema amesema hayo katika mkutano na vyombo vya habari ulioandaliwa na chama chake ambapo aligusia mlolongo wa mambo ikiwemo ujumbe wa Rais Trump kuhusu masuala ya ardhi nchini humo.
“Tunatakiwa kuendeleza lugha moja ambayo itatumika katika bara zima. Mfano Kiswahili, kinaweza kuendelezwa kama lugha kuu ya bara hili.” -Malema
Katika mkutano huo Malema ametaka kuunganishwa kwa bara la Afrika akishinikiza uwepo wa sarafu moja na Rais mmoja.