Mkuu wa Wilaya ya Morogoro DC Regina Chonjo amesema atawachukulia hatua kali wazazi na ndugu endapo mwanafunzi akibebeshwa ujauzito.
DC Chonjo amesema kuwa anatoa wito kwa Madiwani, wazazi na ndugu endapo wakifumbia macho wanafunzi kubebeshwa mimba atawafunga wote.
“Wazazi,ndugu na mwanaume atakayempa mimba mwanafunzi wote nitawafunga,”amesema.
DC Chonjo amesema vijana wengi wa kike wamekuwa wakipata mimba wakiwa shuleni huku jamii yake ikiendelea kufumbia macho suala hilo.