Leo August 30 2018 tunayo story kutoka Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ambapo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Richard Mayongela kuanzisha kitengo cha maalum kutafiti ili kupata viwanja vyote vya ndege nchini vilivyopo chini ya TAA vipatiwe hati.
Nditiye ameagiza TAA ishirikiane na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kutekeleza agizo hilo ili migogoro iliyokuwepo sasa kati ya wananchi na TAA inakwisha.
“Awali nchi nzima kulikuwepo na viwanja 8 vyenye hati, hii ni aibu sasa hivi Mkurugenzi unaniambia viko 11 bado ni aibu, kila Mkoa kuna mgogoro namba tulimalize hili serikali imechoka kulipa fidia kwa viwanja visivyokuwa na hati, wananchi waliopewa viwanja awamu ya kwanza Kipawa na Kigiragira wafanyakazi wa TAA wasio waaminifu walijigawia, ambaye ana kiwanja lakini apokonywe na kufunguliwa mashitaka kusema uongo” Naibu Waziri Nditiye