Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Gaguti ameagiza kusimamishwa kazi Viongozi wa Shule ya Kibeta alipokuwa anasoma Mwanafunzi aliyefariki kwa kuchapwa viboko na Mwalimu wake wa nidhamu.
RC Gaguti amesema tayari wameunda kamati ya uchunguzi ili kufuatilia mwenendo wa shule hiyo, “Nimepata taarifa kuwa Mwalimu alietenda tukio hili amekuwa na tabia ya kuchapa Wanafunzi bila kufuata utaratibu wa adhabu”