Vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) vimeendelea kupata pigo jijini Mbeya baada ya mgombea udiwani katika Kata ya Sisimba kupitia Chama cha NCCR Mageuzi Innocent Siyara kujitoa.
Baada ya kujitoa kwa Innocent sasa kumemfanya mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Geofrey Kajigili kupita bila kupingwa., mgombea huyo amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho ikiwa ni siku chache baada ya mgombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Michael Sanga maarufu kwa jina la ‘Pablo’ kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kukatiwa rufaa na mgombea wa CCM.
Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mbeya, James Cola, alisema ameshapokea barua ya kujitoa kwa Innocent na hivyo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, Kajigili anapita bila kupingwa.
“Ole wenu mtazitapika, ndani ya wiki mbili……..” JPM