Jeshi la polisi Mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Salum Mzee Kondo (38), fundi ujenzi mkazi wa Kidongo Chekundu, Bagamoyo aliyehusika na tukio la mauaji ya mkewe, Mwajuma Omary (27) kisha kutoroka baada ya kutenda kosa hilo.
Mtuhumiwa huyo amekamatwa Septemba 2 mwaka huu Yombo Buza jijini DSM ambako alikimbilia baada ya kufanya kitendo hicho Agost 31,2018, saa 9 alasiri nyumbani kwao Kidongo Chekundu.
Akiweka bayana kuhusiana na tukio hilo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, mtuhumiwa alipokamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kudai alichukua hatua hiyo kutokana na wivu wa kimapenzi.
Alieleza kwamba, mkewe alikuwa akichat na simu huku akiwa anacheka mwenyewe ndipo alipoamua kumnyang’anya simu na kukuta message alizokuwa akichat na mwanaume mwingine.
“Jambo hilo lilisababisha mgogoro kati yao ,ambao ulisuluhishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Magomeni B, lakini marehemu alishikilia kuchoshwa kuishi na mumewe huyo na kuomba kupewa talaka na mumewe aligoma kutoa talaka ” alifafanua Nyigesa.
Pamoja na hilo, Nyigesa alisema wawili hao walikuwa na mgogoro mwingine, uliotokana na mtuhumiwa kuchukua ATM Card ya marehemu mkewe na kwenda kutoa sh.50,000 bila ridhaa yake.
Sayansi ilivyotumika kuondoa mimea yenye sumu Ngorongoro