September 7 2018 wachezaji kutokea taifa la Brazil waliingia katika historia mpya katika Ligi Kuu England, baada ya kiungo wao anayeichezea club ya Tottenham Hotspurs ya England Lucas Moura kutangazwa kushinda tuzo ya mchezaji bora mwezi,
Lucas Moura ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 kwa mwezi August, ushindi huo sasa unamfanya Moura kuwa mchezaji wa kwanza wa kibrazil kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi toka miaka 7 ipite.
Mchezaji wa mwisho wa Brazil kuwahi kushinda tuzo hiyo alikuwa ni David Luis mwaka 2011, hata hivyo Jean Michel Serri wa Fulham FC goli lake alilolifunga dhidi ya Burnley ndio limeshinda tuzo ya goli bora la August.
https://youtu.be/96ABfxSPStA
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe