Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Jumamosi ya September 8 2018 ilikuwa katika wa uwanja wa Nelson Mandela jijini Kampala nchini Uganda kucheza dhidi ya wenyeji wao Uganda ikiwa ni mchezo wao wa pili wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 nchini Cameroon.
Taifa Stars ilikuwa inaingia kucheza mchezo huo ikiwa ina point moja iliyoipata katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Lesotho kwa kutoka sare ya kufungana goli 1-1 Chamazi, wakati Uganda wakiwa na point tatu walizokuwa wamezipata katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Cape Verde.
Uganda na Taifa Stars ukiwa ni mchezo wake wa pili kwa kila mmoja wamejikuta wakitoka sare tasa (0-0), hivyo kwa matokeo hayo Uganda ataongoza kundi lao kwa kuwa na point nne wakati Taifa Stars akiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point mbili lakini wanasubiri mchezo wa kesho kati ya Lesotho dhidi ya Cape Verde kujua msimamo wa kundi hilo utakuwaje.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe