Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli inaendelea na leo September 8, 2018 alikuwa mkoani Simiyu ambapo alimpa nafasi Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola kuzungumza na Wananchi.
Waziri Lugola akizungumza mbele ya Rais Magufuli amesema atahakikisha mafisadi wote wanaenda katika Mahakama ya Mafisadi ili kuwakomesha na kumsaidia Rais kupambana na rushwa.