Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni amezindua operesheni ya ukusanyaji wa mapato ya Jiji la Arusha kwa Wafanyabiashara Jiji hilo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuwahamasisha Watanzania kulipa kodi.
Akizundua operesheni Dkt. Madeni amesema operesheni hiyo imelenga kuhakikisha kuwa kila mfanyabiashara katika Jiji hilo analipa kodi ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kupata huduma bora za kijamii ikiwemo maji, afya na elimu.
Dkt. Madeni amefanya mabadiliko ya kazi kwa msimamizi wa Soko Kuu katika Jiji hilo, John Ruzga kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo mapato ya halmashauri kutokana na soko hilo kukusanya Milioni 23 kwa mwezi badala ya la lengo lililokusudiwa la Milioni 31.6 kwa mwezi na Halmashauri ya Jiji hilo.
“Nimebaini changamoto zilizosababishwa na msimamizi wa soko hili ikiwemo ni pamoja na wamiliki wa vibanda na vizimba kukodisha wafanyabiashara wengine kinyumbe na utaratibu” amesema Dkt. Madeni.
Dkt. Madeni amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu na hivyo aliwataka Watendaji mbalimbali katika Jiji hilo kuhakikisha kuwa operesheni hiyo inafanikiwa ili kuiwezesha Halmashauri hiyo kufikia malengo iliyojiwekea.
Nasari aeleza sababu za kutofanya mikutano katika Jimbo lake ‘nasafiri sana’