Makocha wa kigeni wanaonekana kuendelea kusimamia misimamo yao katika timu zao kwa ajili ya kuimarisha timu kuanzia nje ya uwanja hadi ndani ya uwanja, kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameripotiwa kuwaondoa wachezaji wanne.
Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewaondoa wachezaji wanne wa Yanga kambini kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, Yanga wamewaondoa wachezaji hao na haijaweka wazi watakuwa nje ya kikosi hadi lini.
Wachezaji wanne walioondolewa katika kambi ya Yanga ni golikipa Ramadhani Kabwili, Said Juma Makapu, Haji Mwinyi na Pius Buswita ambao wote wameaondolewa kikosini wakati Juma Mahadhi yeye anakosekana kutokana na kuuguza jeraha lake.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe