Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe leo September 19, 2018 amesema hatoacha Uenyekiti wa Chama hicho mpaka wanachama waliompa dhamana ya uongozi watakapotaka ang’oke.
Mbowe amesema kuwa hataachia uenyekiti kwa kelele zinazopigwa na watu walioko Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mbowe amesisitiza kuwa Uenyekiti wa CHADEMA sio kazi nyepesi wala haina faida na kudai ni kazi ya utume na yenye msalaba kwelikweli ambayo sio kila mtu anaweza kuifanya.
“Hakuna faida kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, huu ni utume, hii ni kazi yenye msalaba, nimepewa mamlaka na Wana-CHADEMA wakitaka Mbowe ondoka kesho, naondoka tena nitashangilia nafanya na sherehe lakini kuambiwa na CCM Mbowe ondoka siondoki” -Freeman Mbowe
CHEKO LA MBOWE: ”WANASEMA NI JIUZULU”