Michuano ya UEFA Champions League hatua ya makundi imeendelea tena usiku wa September 19 2018 kwa game nane kuchezwa, Juventus ya Italiwa wakiongozwa na staa wao raia wa Ureno Cristiano Ronaldo walisafiri hadi Hispania kupambana dhidi ya Valencia.
Juventus wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Valencia, magoli ambayo yote mawili yamepatikana kwa penati dakika ya 45 na 51 penati zikipigwa na Miralem Pjanic, hiyo ni baada ya staa wao Ronaldo kutolewa dakika ya 29 kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Kadi nyekundi aliyooneshwa Ronaldo dakika ya 29 kwa kudaiwa kumsukuma kwa makusudi beki wa Valenci, ndio inakuwa kadi yake ya kwanza nyekundu kuwahi kuoneshwa katika game za UEFA Champions League akiwa amecheza jumla ya mechi 154.
Hata hivyo kwa ujumla katika maisha yake ya soka, Cristiano Ronaldo hii ndio inakuwa kadi yake nyekundu ya 11 kuwahi kuoneshwa katika maisha yake ya soka akiwa Ligi Kuu England na Man United kadi 4, Ligi Kuu Hispania LaLiga akiwa na Real Madrid kadi 4, huku Spanish Super Cup, Kombe la Hispania na Champions League akioneshwa kadi moja moja kila michuano.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe