Nyota ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeicheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, inazidi kung’aa siku hadi akienelea kuitumikia timu hiyo.
Samatta ambaye kwa sasa anashirikia michuano ya UEFA Europa League akiwa na timu yake ya KRC Genk, baada ya kufunga hat-trick katika michezo ya Play off ya Europa League msimu wa 2018/2019, leo aliingia uwanjani tena kuichezea Genk game yake ya kwanza ya Europa League hatua ya Makundi.
Genk usiku wa September 20 walicheza dhidi ya Malmo ya Sweden na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, goli la kwanza la Genk likifungwa na Leandro Trossard dakika ya 37 na Mbwana Samatta akahitimisha kwa kufunga goli la pili dakika ya 71.
Kwa msimu huu ukijumlisha magoli ya Samatta ya Play off anakuwa kaifungia Genk jumla ya magoli sita, kiwango ambacho ni kizuri kwake kujiweka katika nafasi nzuri zaidi, ushindi huo sasa umewaweka Genk nafasi ya pili katika Kundi la kwa tofauti ya goli moja na Besktas anayeongoza Kundi kwa kuwa na point tatu na magoli matatu.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe