Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Serikali itafanya mazishi ya kitaifa na itagharamia gharama za mazishi na kwamba utaratibu kamili wa eneo yatakapofanyika mazishi utatolewa baadaye.
Mpaka sasa zoezi la uokoaji linaendelea huku Vikosi vya mkoani Mwanza vikisaidiwa na vikosi vya mkoa wa Mara.
Aidha, uongozi wa Wakala wa Meli umetambua wafanyakazi wa kivuko watano waliofariki akiwemo Nahodha, Fundi, Karani, Mlinzi na Mkuu wa Kivuko. Kivuko kilikuwa na wafanyakazi 8.
HUZUNI: Miili inaelea, maiti 125 zimetolewa majini, Helicopter ziko hewani