Tamko rasmi la Serikali kuhusu Ajali ya MV Nyerere lililotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijjazi, Dodoma leo. Serikali inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa ndugu waliofarii katika ajali ya MV Nyerere na kuwatakia majeruhi wapone haraka.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi ambapo pia amesema Rais ameagiza Rais Magufuli ameagiza kuwa kufuatia ajali ya MV Nyerere Bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia kesho Septemba 22, 2018
Rais Magufuli ameagiza viongozi wa taasisi na mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini wahojiwe na watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali.
HUZUNI: Miili inaelea, maiti 125 zimetolewa majini, Helicopter ziko hewani