Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ambaye anaichezea club ya Everton ya England kwa saa Theo Walcott, amefunguka na kuelezea magumu aliyopitia dakika za mwisho kabla ya kuihama Arsenal.
Walcott katika mahojiano yake amekiri kuwa alipoteza hamu ya kuupenda mchezo wa soka akiwa Arsenal, hiyo ni baada ya mwaka wake wa mwisho kabla ya kuhama kupata nafasi finyu ya kucheza, kitu ambacho kilimshusha morali na hari ya kujiamini mchezoni.
“Sidanganyi nilijihisi kutokuwa na mapenzi ya mpira tena nikiwa Arsenal, kwa sababu nilikuwa katika kiwango kizuri lakini nilikuwa sipati nafasi ya kuendelea kucheza, kufunga magoli 100 nikiwa na Arsenal ni mafanikio makubwa kwangu ila mwaka mmoja na nusu wa mwisho kabla ya kuondoka nilikuwa na kipindi kigumu sana”
“Siwezi kudanganya ilikuwa ni ngumu kuingia katika timu, nilikuwa naingia na kutoka nilihisi nahitaji kupata hamasa mpya katika soka, sikuwa nikiamini kama inaweza kupatikana nikiendelea kusalia Arsenal”
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe