Baada ya club ya Coastal Union ya Tanga kumsajili staa wa Bongofleva Alikiba katika timu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2018/2019 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, mashabiki wengi walitamani kumuona anacheza mechi za ushindani akiwa na timu hiyo.
Coastal Union hadi sasa imecheza mechi tano za Ligi Kuu bila uwepo wa Alikiba katika kikosi ikiwa imeshinda mechi moja, sare tatu na imepoteza mchezo mmoja ila wengi wameuliza mbona staa huyo haonekani akiichezea timu hiyo mechi za ushindani.
Kocha mkuu wa Coastal Union Juma Mgunda akiongea na Azam TV amelizungumzia suala hilo “Alikiba ni mchezaji wa Coastal Union amesajiliwa kwa uwezo wake wa kucheza, tuna zaidi ya mechi 30 mbele za mashindano na hakika muda ukifika Alikiba atacheza tu, sababu Ali hadi sasa yupo katika list ya wachezaji zaidi ya 12 ambao bado hawajaanza kuitumikia Coastal Union”
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe