September 22, 2018 headlines zimeandikwa kutokea mkoani Mbeya katika fainali za Tamasha la Ngoma za Jadi (Tulia Traditional Dances Festival) 2018 ambayo muasisi wake ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson yaliyofanyika mkoani humo kwa siku tatu mfululizo huku yakishirikisha makundi ya ngoma 135 kutoka Tanzania na moja kutokea Malawi ambapo washindi pamoja na vikundi washiriki wamejipatia zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki na fedha taslim.
Kubwa zaidi washindi hao watapata nafasi ya kujiunga na mafunzo ya sanaa katika chuo cha sanaa Bagamoyo lakini pia watapata nafasi ya kushiriki katika matamasha mbalimbali makubwa nje ya nchi ikiwemo India na nchi nyingine jirani.
Ngoma za Dr. Tulia zilivyosimama kwa muda kuomboleza msiba