Kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa Mkuu wa Kituo hicho mkoani Arusha, Shilinde Ngalula kimesema kwamba taarifa za mapato na matumizi hayapelekwi TAKUKURU kama ilivyodaiwa bali taarifa zake zinapelekwa Brela kwa mujibu wa sheria.
Ngalula amesema “Hakuna sheria inayotoa maelekezo kuwa asasi za kiraia kupeleka maelekezo TAKUKURU, sisi tunaongozwa na sheria za makampuni, sisi tunatoa taarifa Brela, hakuna mahala kuna sheria inaelekeza tutoe taarifa TAKUKURU”