Leo September 28, 2018 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana na kuzungumza na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.
Prince William ambaye aliwasili nchini Septemba 26, 2018 kwa ziara maalum ambapo awali alikutana na Rais Magufuli na baadae kupokelewa ofisini kwa Waziri Kigwangalla, amesema kuwa amefurahia uwepo wake hapa nchini hali iliyopelekea kukaa kwa muda huo tofauti na Nchi zingine ambazo amekaa kwa siku moja.
Prince William ameweza kumtembelea Dk. Kigwangalla katika ofisi ndogo ya Wizarani ambapo katika mazungumzo baina ya wawili hao, ikiwemo suala la kuomba msaada wa kusaidia Sekta ya Utalii.
“Kiukweli tokea kumpokea hapa Nchini alipoingia Septemba 26, Prince William amefurahia ..na nimeweza kumuomba msaada wa masuala mbalimbali ya kusaidia Sekta ya Utalii na Uhifadhi wa Nchi yetu kutokana na yeye kuwa na mapenzi ya kipekee kwenye uhifadhi na pia anakumbukumbu nzuri na Tanzania kiasi cha kukaa siku tatu hapa tofauti na nchi zingine alizokaa siku moja” ameeleza Dkt. Kigwangalla.
“lengo la kumuomba atusaidie katika kujenga makumbusho ya kuhifadhi meno ya tembo ni kutokana na Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za awali tano za Afrika kusaini mpango wa kulinda tembo kule nchini uingereza mwaka 2008″ Kigwangalla
Dkt. Kigwangalla alimuomba Prince William msaada wa ndege aina ya Helkopta Nne, ikiwemo mbili zitakazokuwa kwa ajili ya dharura na mbili zingine kwa ajili ya doria kwenye baadhi ya maeneo ya uhifadhi nchini.
Prince William na ujumbe wake huo umeweza kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na pia Chuo cha Wanyamapori cha Mweka (College of African Wildlife Management, Mweka (CAWM), kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na baada ya hapo ataendelea na ziara yake Nchini Kenya.
RC Mbeya achafukwa na mradi uliotengenezwa kihuni “DC, Mkurugenzi nanyi mpo mmeupokea”