Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amekemea utaratibu wa watuhumiwa kunyimwa dhamana hasa siku za mapumziko kwa kisingizio kuwa si siku za kazi.
Akizungumzakatika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Busanza wilayani Uvinza mkoani Kigoma, Lugola amesema dhamana kwa mtuhumiwa inapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki.
Amesema vituo vya polisi nchini vinafanya kazi siku zote za wiki zikiwemo za mapumziko, kuahidi kutomfumbia macho askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana.