Leo October 2, 2018 Nakusogezea taarifa kutoka Menejimenti ya Chuo Kikuu cha St Johns cha Tanzania, yaani, St Johns University of Tanzania (SJUT), ambapo inapenda kuutaarifu umma na Watanzania kwa ujumla kuwa Chuo Kikuu hicho kilichoko Kikuyu, Jijini Dodoma, HAKIJAFUNGWA wala HAKIJAFUTWA na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Aidha Menejimenti inafafanua kuwa kilichofutwa ni Senta yake ya Msalato baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuridhia maamuzi ya Baraza la Chuo Kikuu hicho kuifunga Senta hiyo.
Menejimenti inachukua nafasi hii kuwatakia maandalizi mema wanafunzi wote waliopata udahili katika programu za Shahada katika fani za Uuguzi, Ufamasia, Ualimu wa Sayansi na Ualimu wa Sanaa, na pia katika programu za Certificate na Diploma katika fani mbalimbali, za St Johns University of Tanzania. Wanafunzi wapya wanashauriwa kutembelea tovuti ya Chuo Kikuu hicho mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi. Tovuti ya St Johns University of Tanzania ni www.sjut.ac.tz. Pia wanaweza kupiga simu namba 0754 285 909 au 0712 882 734.
Imetolewa na Prof Emmanuel Mbennah, Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha St Johns cha Tanzania, Jijini Dodoma.
Prof Emmanuel D Mbennah, Ph.D., Ph.D.
Vice Chancellor,
St Johns University of Tanzania
P.O Box 47, Dodoma, Tanzania.
Tel: 026-239 0044 | Fax: 026-239 0025 | E-mail: admin@sjut.ac.tz | Website: www.sjut.ac
“Nilipokea kwa huzuni taarifa ya Rais alipomteua Diwani kuwa Boss TAKUKURU” RC Kagera