Leo Oktoba 6, 2018 nakuletea stori kutoka huko Mkoani Lindi ambapo Hoteli ya Star com ya Mkoani Lindi ambayo ni maarufu kwa Wasafiri kutoka katika Mikoa ya Kusini kuelekea Dar es salaam kujipatia chakula imeteketea kwa moto majira ya saa kumi jioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatah Mzinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa chanzo cha moto huo umetokana na Mtu ambae hajafahamika mpaka sasa kuchoma kichaka kilichokuwa karibu na Hoteli hiyo na kisha upepo mkubwa kupuliza moto huo na kufanya cheche za moto kurukia katika paa la Hoteli hiyo na kuiteketeza.
Inaelezwa kuwa vitu vya thamani vimeteketezwa kutokana na moto huo huku hakuna Mtu yeyote aliyedhuhurika na moto huo na wala hakuna Mtu yeyote aliyekamatwa kutokana na tukio hilo.
Aidha Kamanda Renatha amewataka Wananchi kuacha tabia ya kuchoma hovyo vichaka hasa vile ambavyo vipo karibu na makazi ya Binadamu.
Daktari feki aliekamatwa Mwanza akiri “Tuliambiwa Bugando imechafuka, inanuka”