Mwisho wa wiki iliyopita kuna taarifa ambazo ilitoka kutokea Bukoba mkoan Kagera inaeleza kuwa TCRA ina watahadharisha “wasimamizi ‘Admin’ wa makundi ya Whatsapp yaliyoundwa kwenye simu za mkononi kwa kutosimamia maadili ya wanachama.
Makundi hayo ambayo huanzishwa kwa lengo mahususi yanatumika kama majukwaa ya mijadala, maelekezo ya kazi hata malumbano huku aliyeunganishwa akiwa na uhuru wa kujitoa kwenye kundi.
Onyo la TCRA dhidi ya wasimamizi wa makundi hayo limetolewa leo Oktoba 5 mjini Bukoba na ofisa wa mamlaka hiyo, Francis Mihayo wakati wa semina kwa viongozi wa mkoa wa Kagera.
Amewataka wasimamizi hao wa makundi hayo kutoogopa kuwaondoa wanachama wao wanaokiuka maadili kwa kuwa wao kama wasimamizi wanaweza kuchukuliwa hatua na mamlaka hiyo”.
AyoTV imempata wakili wa kujitegema Jebra Kambole ametoa ufafanuzi wa sheria ya kimtandao.
DIWANI CHADEMA: Kakaa Jela Miezi 10 kafunguka ”Nilionewa”, Bonyeza play hapa chini kutazama