Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kukamata gari ya Kampuni ya Oil Com likiwa limebeba vipodozi ambavyo vilikuwa vikiingizwa nchini kimagendo pamoja na pombe kali likitokea nchini Zambia na dereva wa gari hilo alikimbia na amejulikana kwa jina la Michael Godson.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda Ulrich Matei amesema gari hilo limekamatwa wakati Polisi wakiwa kwenye doria na tayari Mmiliki wa gari ameshapatikana.