Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla amesikiliza kero mbalimbali katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kama alivyoweka utaratibu wakusikiliza wanannchi, lakini pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya ya Mpanda na Tanganyika kutatua Kero zote zilizowasilishwa.
Makalla amepokea kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kero za ardhi pamoja na kudhurumiwa mali mbalimbali kama nyumba na fedha.
Ambapo RC Makalla amewaagiza Wakuu wa wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando na Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matiga kushughulikia na kutatua kero zote ambazo zimewakilishwa mbele yao.
Huku akitoa agizo kwa idara ya ardhi kuhakikisha wanawashughulikia wananchi wote wenye matatizo ya ardhi waliyoyawasilisha katika kikao hizo.
Mwanzilishi wa Nursery DSM afunguka”nilianza fundisha tuition, sasa namiliki Shule Tatu kubwa”