Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumanne ya October 16 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam iliwakaribisha timu ya taifa ya Cape Verde katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019 nchini Cameroon.
Taifa Stars walikuwa nyumbani baada ya game ya kwanza iliyochezwa October 12 2018 mjini Praia Cape Verde, walipoteza kwa magoli 3-0, hivyo matumaini yakaanza kupotea baada ya wao kuwa nafasi ya mwisho, Taifa Stars leo wamebadili matokeo na kufanikiwa kulipa kisasi kwa kuifunga Cape Verede kwa magoli 2-0.
Magoli ya Taifa Stars yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 29 baada ya kupokea pasi safi ya nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na goli la pili lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 57 kwa kutumia vyema pasi ya Mudathir Yahaya.
Ushindi huo sasa unaifanya Taifa Stars irudi nafasi ya pili kwa kufikisha jumla ya point tano wakifuatiwa na Cape Verde waliokuwa na nafasi ya nne huku Uganda bado anaongoza Kundi L kwa kuwa na point 7 huku game yake na Lesotho ikiendelea kama ikimalizika kwa ushindi Uganda atakuwa na point 10.
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga