Stori inayotrend Tanzania kwa sasa ni kumhusu Mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu MO ambaye ametekwa na mpaka sasa hajapatikana na Familia yake imetangaza dau la Bilioni moja kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwake.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika katika Instagram page yake hivi namnukuu “Jambo la mwisho kwa leo, ni la kawaida kwenye mambo ya Uchunguzi, ni ganda la risasi ambayo ilitumika. Limeokotwa na Polisi? Kinachoitwa ‘ballistic report’ kimetolewa na kusambazwa duniani kwenye kanzidata za watengeneza silaha?”
“Hii ingesaidia sana kuweza kujua umiliki wa silaha iliyotumika na kuwa na njia ya kuwapata watekaji na pia kumpata MO. Jeshi la Polisi likipata msaada kutoka nje ya nchi laweza pia kufanikisha hili.” -Zitto Kabwe
“Mwisho, kumekuwa na kauli za kusema kuwa ‘wanasiasa wasitake umaarufu’ kwenye tukio hili. Hii ni kauli ya hovyo na inapaswa kupuuzwa. Mamlaka za Serikali zimejengwa kusimamiana. Waziri Kivuli Godbless Lema ana wajibu wa kumhoji Waziri wa Mambo ya Ndani bila kuonekana anaingiza Siasa.” -Zitto Kabwe
“Hakuna kipindi Serikali imepewa fursa ya kupumua kwenye tukio kama tukio hili la kutekwa kwa Mohammed Dewji. Wanasiasa wa upinzani tulikaa kimya kupisha vyombo kufanya kazi zake. Serikali kuanza kuweweseka pale wabunge wanapotimiza wajibu wao kuhoji kunatia mashaka Kwamba kuna kitu Serikali inaogopa. Serikali inaogopa nini? Wanachokiogopa Ndio kinaogopesha kukaribisha Wachunguzi wa Kimataifa?” -Zitto Kabwe
MAGAZETI LIVE: Kutekwa kwa MO bado utata, Mwakasege asimulia safari ya Mwanae kabla kifo