Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 3 likiwemo kuiisababishia TPA hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 150.
Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa serikali kutoka TAKUKURU, Lizy Kiwia, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi inadaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo October 25, 2012.
Anadaiwa akiwa katika Ofisi Kuu za TPA zilizopo, Temeke mshtakiwa huyo wakati akijua kuwa ana nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722A kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. Akidai kuwa, gharama ya Semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. MIL 47.9 wakati akijua alikuwa na lengo la kumdanganya muajiri wake huyo TPA.
Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa huyo wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722B kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd akidai kuwa, gharama ya Semina ya siku tatu ilikuwa ni sh.MIL 47.9 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.
Katika shtaka la tatu mshtakiwa anadaiwa, December 5, 2012 akiwa TPA alitumia hati ya malipo namba MKOO/1203 Kutoka huko huko Bob yenye gharama ya Sh.MIL 97.
Shtaka la nne imedaiwa kati ya Oktoba 30 na Desemba 12/2012 huko TPA, mshtakiwa kwa nia ovu aliisababishia TPA hasara ya Sh.MIL 158.9.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo, ambapo amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 wenye barua za utambulisho.
Pia, Hakimu amesema mshtakiwa atatakiwa kuweka nusu ya fedha hizo au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi imeahirishwa hadi hadi October 29, 2018 kwa kutajwa na kuangalia upelelezi umekamilika au la.
MAGAZETI LIVE: Kutekwa kwa MO bado utata, Mwakasege asimulia safari ya Mwanae kabla kifo