Leo October 17,2018 tunayo Exclusive story kutokea kwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk.Wilbroad Slaa ambapo amezungumzia suala la ajira kwa nje ya nchi na hapa nchini.
Dk.Slaa amesema wakati akiishi Canada na Stockholm kufanya kazi zaidi ya moja ni jambo la kawaida.
Amesema mtu anaweza kufanya kazi ofisini na anatoka kwenda kufanya kazi za usafi na muda mwingine kazi za usafi zinakuwa na mshahara mzuri kuliko za ofisini.
“Lazima tubadilishe mawazo yetu ambapo falsafa ya Hapa Kazi iwe kwa vitendo, kwani kazi haichagui. Unapozungumzia ajira hata shambani ni ajira, hata kusukumiza mkokoteni ni ajira hivyo watu wabadilishe mawazo,” amesema Slaa.