Tumezoea kukutana wakandarasi wengi nchini na nje ya nchi wakitumia skaveta ambazo zinatumia mafuta ili ziweze kufanya kazi ya kuchimba mashimo au barabara,
Elia Daniel Kasanga ni kijana wa kitanzania aishie Wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora ambaye ametengeneza Skaveta ndogo ambayo inatumia umeme wa betri huku ikifanya kazi sawa na ile inayotumia mafuta.
Elia anasema kuwa wazo la kutengeneza Skaveta hiyo alipata baada ya kuona skaveta zinazotumia mafuta hutumia gharama kubwa zaidi ya mafuta ambapo hutumia mpaka lita 200 kwa kazi za migodini lakini yeye anasema kuwa yake haitumii mafuta hata kidogo na haitakuwa na gharama yeyote akiwezeshwa kutengeneza kubwa zaidi ya kufanya kazi kama za migodini.
Elia anasema ilimchukua mwaka mzima kutengeneza Skaveta hiyo ambayo alitumia wepa za gari na vyuma ambavyo aliunganisha akiwa katika karakana yake ya kuchomelea vyuma iliyopo wilaya ya Urambo Tabora na kumgharimu kiasi cha Milioni moja za Kitanzania.