Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo Jumamosi ya October 20 2018 kwa michezo kadhaa kucheza, club ya Dar es Salaam Young Africans ilikuwepo uwanja wa Taifa DSM kucheza dhidi ya Alliance ya Mwanza.
Yanga ikiwa katika uwanja huo inaoutumia kama uwanja wake wa nyumbani, imefanikiwa kuiadhibu Alliance FC iliyopanda daraja msimu huu, kwa magoli 3-0, magoli ya Yanga yakifungwa na Herieter Makambo dakika ya 18, Mrisho Ngassa dakika ya 25 na Ibrahim Ajib dakika ya 86.
Ushindi huo sasa unaipeleka Yanga SC katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019, Yanga sasa wanapoint 19 nyuma ya Azam FC wanaongoza Ligi kwa kuwa na point 21 lakini wameizidi Yanga miwili, Azam FC wakiwa wamecheza game tisa na Yanga saba.
Wapinzani wa jadi wa Yanga ambao ni Simba SC wao wapo nafasi ya sita wakiwa wamecheza game sawa na Yanga ila wao Simba wanapoint 14 na watashuka dimbani kesho kucheza dhidi ya Stand United, Ibrahim Ajib ameendelea kuonesha uwezo wake wa kufunga magoli mazuri.
Samatta alivyofutwa miguu baada ya game