Leo October 22, 2018 Walimu wawili Elieth Gerald na Respicius Mtazangira wanaoshtakiwa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia kwa aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya msingi Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba kesi yao imeanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama kuu kanda ya Bukoba.
Ambapo kupitia kesi hiyo, washtakiwa wamekana kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya mwanafunzi huyo huku Mwalimu Respicius akikubali kuwa alitoa adhabu ya viboko sita lakini havikusababisha kifo chake. Kesi hiyo imehairishwa hadi kikao kingine cha Mahakama Kuu kitakapofanyika.