Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo Jumatatu ya October 22 2018 ametangaza kuwatafuta vijana waliosoma masuala ya IT kwa ajili ya kusaidia ufungaji wa system ya kuripoti, kutoa maoni na kujua uwajibikaji wa kila mtumishi kuanzia ngazi ya mtaa.
RC Makonda anawaalika wote wenye utaalamu wa Teknolojia ya IT kufika Ofisini kwake November 1 2018 Asubuhi kwa ajili ya kuunda Mfumo wa kuratibu Uwajibikaji wa Watendaji wa Umma ilikuhakikisha malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa uharaka.
Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na viongozi Wakuu akiwemo Mkuu wa mkoa, Katibu tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara Watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua kero za wananchi.
Lengo la RC Makonda ni kuondoa adha kwa wananchi wanaokwenda kuhudumiwa katika ofisi za Umma na kuambia “Njoo kesho” kila siku pasipokujua kuwa wanatumia nauli na kupoteza muda wao, mfumo huo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.
Taarifa kuhusu Waziri January Makamba kuitwa Polisi kisa tukio la Mo Dewji