Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeendelea tena uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC kuikaribisha Yanga SC kucheza mchezo wao wa nane wa Ligi Kuu kwa Yanga na KMC ukiwa wa 11.
Yanga akiwa kama timu mgeni uwanja wa Taifa Dar es Salaam alipambana kuhakikisha anapata ushindi lakini mambo yalikuwa tofauti na KMC walionesha nidhamu nzuri ya ukabaji kwa dakika 88 za mchezo.
Makosa yaliofanywa na mchezaji wa KMC dakika za lala salama ndio yameihukumu KMC dhidi ya Yanga kwani walifanya madhambi mita chache kabla ya goli na faulo ikapigwa na Feisal Salum Fei Toto na kuifanya Yanga kupata ushindi wa goli 1-0 dakika ya 89.
Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe jumla ya point 22 na kuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu msimu huu nyuma ya Azam FC iliyopo nafasi ya kwanza kwa kuwa na point 22 ikiizidi Yanga michezo miwili mbele, KMC wao wapo nafasi ya 15 wakibaki na point 10 wakicheza michezo 11.
“Tumeshinda ili kuweka tabasamu usoni kwa MO Dewji”-Kocha Simba SC