Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itaweka kambi ya siku kadhaa nchini Afrika kusini kabla ya kucheza dhidi ya Lesotho katika mchezo wa mzunguuko wa tano wa Kundi L wa kuwania kufuzu AFCON 2019.
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe leo ametangaza mkakati huo katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya harakati za kuhakikisha Taifa Stars wanapata matokeo dhidi ya Lesotho.
“Rais wetu kama kawaida yake aliongoza kwa mfano alikabidhi Tsh Milioni 50 za maandalizi ya mechi ya marudiano dhidi ya Lesotho na kutuagiza wote tuliopo katika uongozi kuwa kuhakikisha tunashinda mchezo huo”>>>Dr Mwakyembe
“Tukifanikisha hilo Mh Rais ameahidi kuwa atajiunga nasi uwanjani siku ya mechi ya marudiano na Uganda, changamoto aliyotupa Rais imetufanya tufikirie nje ya sanduku, ndg zangu hivyo tumeona sio busara kutoka na timu hapa moja kwa moja hadi Lesotho hivyo tunaona ni bora kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini ili timu izoee hali ya hewa ya nchi za Kusini”>>> Dr Mwakyembe
Waziri mwakyembe amesema tathmini iliyofanywa na shirikisho la soka Tanzania TFF kuelekea mchezo huo, imebaini Taifa Stars italazimika kuondoka nyumbani mapema na kwenda nchi jirani na Lesotho kwa ajili ya kuweka kambi ili isaidie wachezaji kuizoea hali ya hewa ya kusini mwa Afrika.
“Tumeshinda ili kuweka tabasamu usoni kwa MO Dewji”-Kocha Simba SC