Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Hassan Suluhu ametembelea mradi wa ujenzi wa Tenki la maji la Bagamoyo lililojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DSM (DAWASA).
Mama Samia akiwa katika ziara ya siku tano Mkoa wa Pwani kuanzia Oktoba 24 hadi 29 atatembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Kisarawe ulio chini ya Mamlaka hiyo.
Akielezea mradi huo kwa Makamu wa Rais, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa mradi huu ni msaada kutoka Benki ya Exim unaotarajiwa kukamilika Desemba Mwaka huu.
Kwenye mradi huo wa Bagamoyo, Mama Samia ametembelea ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni 6 kwa siku likiwa ni moja kati ya mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.
Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ulianza rasmi mwezi Machi mwaka 2016 na utakamilika 2018.
Kubwa zaidi ni pale Mbunge was Jimbo la Bagamoyo Dr. Shukuru Kawambwa alipofikisha ombi kiutani kwa Makamu wa Rais wa Tanzania kuhusu mradi wa maji ambao umejengwa katika mji wa Bagamoyo lakini hauwafikii wananchi, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na Mtendaji mkuu wa DAWASA walivyomjibu.
MWILI WA MWANZILISHI WA TUKUYU STARS WAAGWA NA KUCHOMWA MOTO
https://youtu.be/sjALbcc1uLc