Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa wa Pwani kukagua shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali,
Moja ya sehemu ambapo ametembelea ni katika Jimbo la Chalinze linaloongozwa na Mbunge Ridhiwani Kikwete ambaye alimwambia Makamu wa Rais Mama Samia kuwa tatizo la maji katika jimbo hilo lina zaidi ya miaka 13 mpaka kufikia wananchi kutotamani kusikia tena maneno kuhusu maji bali kutaka kusikia maji yanatoka.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Eng. Cyprian Luhemeje aliahidi kwa wakazi wa Chalinze kuwa mpaka kufikia december 31 ya mwaka huu maji katika Mji wa Chalinze yatakua yanatoka na tatizo la maji katika mji huo litakua limetatulika kabisa.
Kwa upande wake Makamu wa Rais akijibu hoja ya Ridhiwani Kikwete amesema wao wakiahidi hutekeleza hivyo waliwaahidi wakazi wa Chalinze kuwa wanawaletea maji na yatafika December 31 mwaka huu wasiwe na wasiwasi.
MWILI WA MWANZILISHI WA TUKUYU STARS WAAGWA NA KUCHOMWA MOTO
https://youtu.be/sjALbcc1uLc