Naibu Spika Dr Tulia Ackson alifunga safari kutoka mkoani Dodoma hadi katika Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida ambapo aliendesha harambee ya ukusanyaji pesa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani humo.
CCM kwa kushirikiana na Serikali na wananchi, inatekeleza miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa, ujenzi wa vibanda vya biashara 8 na Choo cha kulipia katika stendi ya Wilaya pamoja na ujenzi wa Hoteli ya kisasa. Miradi hiyo inakadiriwa kugharimu zaidi ya Shilingi Billion 1.8 hadi kukamilika kwake na katika harambee hiyo zaidi ya Shilingi Milion 61 zilipatikana.
VIDEO: Bodi ya filamu ilivyomfungia Wema Sepetu kisa video yake na ‘Future Husband’