Golikipa wa klabu ya FC Barcelona Victor Valdes alishatangaza tangu msimu uliopita kwamba hatoongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo na kwamba angeondoka Nou Camp baada ya msimu huu ambapo wakati Barca wakiwa wanasaka mrithi wa Valdes, nahodha wa klabu hiyo Carles Puyol nae ametangaza ataondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu kwa sababu anahitaji kupumzika.
Puyol ambaye alianza kuichezea Barca tangu utoto wake, ni mchezaji wa pili kwa kuichezea mechi nyingi klabu hiyo baada ya Xavi ambapo anasema baada ya kupumzika kwa muda ataamua wapi aende kuendeleza maisha yake ya soka.