Club ya Real Madrid ya Hispania usiku wa Jumatatu ya October 28 2018 imetangaza maamuzi magumu kuhusiana na club yao, club ya Real Madrid ikiwa imepita siku moja tu baada ya kupoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya FC Barcelona katika game ya EL Clasico uwanja wa Nou Camp.
Leo imetangaza maamuzi magumu ya kuamua kumfuta kazi kocha wake mkuu Julen Lopetegui kutokana na mfululizo wa mwenendo mbaya wa timu hiyo, Lopetegui amefutwa kazi na nafasi yake imechukuliwa kwa muda na Santiago Solari ambaye ni kocha wa timu ya akiba ya Real Madrid.
Lopetegui anafutwa kazi ikiwa imepita miezi minne tokea atangazwe kuwa kocha mkuu wa club hiyo, baada ya kufutwa kazi timu ya taifa ya Hispania siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya World Cup 2018, sababu kubwa ikitajwa ni kutoka kwa taarifa za kujiunga Real huku viongozi wa chama cha soka Hispania kikiwa hakifahamu.
Kwa sasa Real Madrid ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa LaLiga msimu huu wa 2018/2019 ikiwa na point 14, Barcelona wakiongoza Ligi kwa point 21, Real ikiwa chini ya Lopetegui imecheza jumla game 14, ameshinda game sita, sare game mbili na kapoteza game sita na ameruhusu magoli 20 na kufunga 21.
Angalia Mwakinyo alivyoendeleza ubabe, kampiga Sinkala TKO round ya pili