Leo October 30, 2018 Mkuu wa mkoa wa Katavi Amosi Makala ameamuru kuachiwa kwa mabasi kumi yaliokuwa yakishikiliwa na maafisa uvuvi Kanda ya Magaharibi katika kituo cha polisi Mpanda kwa kudaiwa kusafirisha samaki kinyume na utaratibu.
Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo na malalamiko ya wananchi ya kukosa kitoweo cha samaki katika masoko mbalimbali ya mikoa ya Rukwa na Katavi .